Über uns

Tangu mwaka 1992 Parokia ya Luther-Melanchthon Lübeck / Ujerumani imekuwa na mahusiano na Parokia ya Igoma Lutherani huko Mwanza / Tanzania.

Parokia yetu ipo kusini mwa wilaya ya Lübeck. Ina wanadamu 6000. Kanisa la Kilutheri ni makao makuu. Lili jengwa kipindi cha utawala wa Manazi kama makao makuu pekee katika Lübeck. Hivyo basi lipo katika uangalizi maalumu.

Parokia ya Igoma Lutherani ipo Igoma / Mwanza. Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa Tanzania. Limepakana na ziwa Victoria. Kuna parokia nyingine ndogo ndogo katika wilaya tofauti za Mwanza na sharika katika vijiji vya Ikengele, Ihayabuyaga na Kissesa nje ya mji. Makanisa mawili makubwa na matatu madogo katika usharika yapo chini ya Parokia ya Igoma. Wakristo wa Mwanza wanatoka katika jamii tafauti. Washarika wengi wanatoka katika jamii za vijiji, wanaishi maisha duni kutegemea kile wanacho zalisha katika mashamba yao.

Sehemu nyingine muhimu ya ushirikiano ni Dayosisi ya mashariki mwa ziwa Victoria. Ina nufaika katika ushirikiano huu. Makao makuu ya dayosisi ni Mwanza.

Kwa kushirikiana na washirika wetu, tunajishugulisha na miradi miwili:

Maandalizi ya uzazi: tunawasaidia wanawake wajawazito, kwa kutoa vifaa salama, madawa, misaada na usafiri kwenda hospitali. “Kuwasaidia watoto wenye matumaini”: Watu wa Ujerumani, wana wasaidia watoto wa Igoma kwenda shule.

Timu yetu

Kikundi cha ushirikiano Lübeck, kinafanya kazi za ushirikiano huo. Kamati ya ushirikiano Lübeck na Kamati ya ushirikiano Igoma zinafanya kazi za ushirikiano